Habari za Mastaa

DJ Khaled anaweza biashara? Itazame hii mpya kutoka kwake:’Miami Finga Licking’ + (Video)

on

finga lickin

DJ Khaled anaziandika headlines kwenye biashara tofauti, licha ya kutengeneza pesa ndefu kwenye muziki peke yake Dj na rapper huyu kutoka ‘We The Best Music’ ameona itakuwa poa zaidi kama akiendelea kuwekeza pesa yake kwenye vitu vingine tofauti na muziki.

Miami Finga Licking Restaurant ndio headlines anazoziweka Dj Khaled jijini Miami, kwa kuwa kila kitu anachokigusa Dj Khaled ni ‘The Best’ rapper na Dj huyo ameona sio mbaya akiwekeza kwenye biashara tofauti na time hii hela yake kubwa ameamua kuiwekeza kwenye biashara ya msosi.

finga lickin4

Muonekano wa restaurant ya Miami Finga Licking ya Dj Khaled

Kwenye interviews zaidi ya moja DJ Khaled ameshasikika akielezea jinsi gani ambavyo anapenda msosi na msosi aupendao kuliko chakula chochote ni wali nyama na samaki na kwenye restaurant yake ya Miami Finga Licking vyakula hivi ni lazima ukutane navyo kwenye menu.

finga lickin2

Vyakula kama hivi utavipata kwa Dj Khaled mtu wangu.

Miami Finga Lickin Restaurant ipo maeneo ya Miami Gardens na ni miongoni mwa restaurant kubwa zilizofunguliwa maeneo hayo au kama Dj Khaled anavyopenda kusema; ‘We The Best Restaurant’.

Hapa chini nimekuwekea baadhi ya picha nilizoweza kuzinasa..

miami2

Dj Khaled anapenda wali mtu wangu, so lazima utakutana na wali kwenye menu.

miami1

Mambo ya jikoni ndio kama hivi

miami6

Watu walikaribishwa kwenye uzinduzi wa biashara hii mpya ya Dj Khaled kujipatia msosi mzuri.

miami4

Dj Khaled alikuwepo kuwakaribisha watu na kuwaonyesha watu muonekano wa biashara yake mpya.

miami5

finga lickin3

Huyu ni Chef mkuu wa restaurant ya Dj Khaled.

Hapa nimekusogezea kipande cha video ya restaurant hio mpya ya DJ Khaled karibu uweze kuitazama mtu wangu.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments