Top Stories

Maneno ya Dk. Magufuli ndani ya dakika 18 baada ya kupokelewa na watu wa Dar es Salaam… (Audio)

on

Screen Shot 2015-07-14 at 4.35.33 PM

July 14 2015 Dar es Salaaam imemkaribisha Mgombea Urais ambaye amepitishwa na CCM pamoja na Mgombea Mwenza… Hii ilikuwa safari ya kutambulishwa Mgombea Urais John Pombe Magufuli pamoja na Samia Suluhu Hassan ndani ya Dar baada ya Kikao Kikuu cha Halmashauri ya CCM kuwapitisha Wagombea hao Makao Makuu ya Chama, Dodoma Tanzania.

Dk.-John-Pombe-Magufuli-620x308

Naomba nirudie kushukuru Wajumbe wa Mkutano wa Taifa ambao waliamua kunipitisha niwe Mgombea wa Urais nikiwakilisha CCM, ninawashukuru sana… Nilipokuwa nachukua na kurudisha fomu mara nyingi nilikuwa nazungumza neno moja, ninaomba Watanzania waniombee…

Kupitishwa kwangu na Kamati Kuu inadhihirisha mlikuwa mnaniombea na nataka niseme kwa dhati sitawaangusha, nitafanya kazi kwelikweli kama nitapewa ridhaa kuiongoza hii nchi sitaogopa mtu na wala sitapenda mtu wa chini aonewe kwa sababu maonevu yamekuwa yapo.”

unnamed (43)

Dk. Magufuli kwenye moja ya mojawapo ya majukumu yake ya sasahivi Wizara ya Ujenzi.

Nitahakikisha ninaisimamia vizuri Serikali ili kero ndogondogo ziweze kufutika.. ndugu zangu sikuja kufanya Kampeni nilikuja kujitambulisha, jina langu ninaitwa John Pombe Joseph Magufuli.” >>> Dk. Magufuli.

Katika Mchakato wa Chama tulikuwa Wanachama 42, na kulikuwa na Makundi 42 na Makundi katika Kugombea sio makosa hasa kwa chama kama CCM, baada ya Mchakato wote tumeungana na sasa tumekuwa group moja la CCM

Ninazungumza jua linawaka haki ya MUNGU kweli tutafanya kazi, ninawaomba mkiamini Chama cha Mapinduzi, niwaombe tushikamane kwa pamoja sura yangu ni mbayambaya lakini saa nyingine inakuwaga nzuri usiku, sura ya tabia ni nzuri lakini mnachohitaji ni kazi, maendeleo na kuondolewa kero zao.. mimi sio mkali ila nawachukia watendaji ambao hawatimizi wajibu  wao, na hao ndio nitalala nao mbele.“>>> John Magufuli.

Magufuli-from-CCM

Utamsikiliza hapa Waziri Magufuli wakati akiongea na watu wa Dar baada ya Mapokezi yake July 14 2015.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments