Rais Msitaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mapema leo February 8, 2025 amewasili wilayani Bukombe Mkoani Geita na kuweka Jiwe la Msingi katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Bulangwa .
Akiweka Jiwe hilo la Msingi Dkt. Kikwete amewapongeza wananchi wa Bukombe kwa ushirikiano wanao utoa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa vipaumbele katika sekta ya Elimu wilayani humo.
Rais Msitaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameambatana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko katika kuweka jiwe la Msingi ambapo Dkt. Biteko amempongeza Rais Msitaafu Kikwete kwa kujenga ukumbi huo kwa manufaa ya wanafunzi na wananchi wa Bulangwa.
Akisoma taarifa ya Ujenzi wa ukumbi huo Mkuu wa Shule ya Sekondari Bulangwa Bi. Sane Elizabeth Machembe amesema ujenzi wa ukumbi huo umefikia asilimia 85 na unatarajia kuhudumia watu 3500 hadi 4000 kwa wakati Mmoja.