Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka wananchi wa mkoa wa Tanga kutunza na kulinda mazingira kwa kuepuka vitendo vya ukataji miti ovyo na uchomaji wa misitu hali inayoharibu uoto wa asili na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Akizungiumza na wakazi wa Kabuku wilayani Handeni, Dkt. Mpango amesema uharibifu wa mazingira unaathiri uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara mkoani Tanga kwani unasababisha ukame na mvua nyingi zisizo na msimu na hivyo kuharibu barabara.
“Hakikisheni mnatunza na kulinda mazingira ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kurejesha thamani ya mkoa wa Tanga katika uzalishaji wa mazao hususan mahindi, matunda na mboga za majani amesisitiza Dkt. Mpango.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Wizara kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Tanga umejipanga kuhakikisha barabara ya Handeni –Mafuleta Km 20 ujenzi wake unaendelea kwa kasi ili kufidia muda uliopotea kutokana na changamoto za mkandarasi.
Aidha, Eng. Kasekenya amesema kuhusu kuunganisha mkoa wa Tanga na Morogoro kupitia barabara ya Handeni-Mziha-Turiani km 108.2, tayari kibali cha ujenzi huo kimepatikana na ujenzi wake utaanza hivi karibu