Waziri wa Katiba na sheria Dokta Damas Ndumbaro amewataka waajiri wapya mawakili na makatibu sheria ofisi ya taifa ya mashitaka kuhakikisha wanakua mwarobaini kutatua changamoto ya migogoro ya Wakulima na Wafugaji nchini.
Dokta Ndumbaro ameyasema hayo mjini Morogoro wakati akifungua mafunzo ya elekezi kwa waajiri wapya 215 kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambapo amesema maeneo mengi ya nchi yanakabiliwa Changamoto ya Migogoro ya wakulima na Wafugaji hivyo ofisi hiyo inawajibu mkubwa kukomesha changamoto hiyo.
Anasema endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake kuna uwezekana changamoto hii kumalizika kabisa licha ya kuwepo kwa miaka mingi na kuleta madhara makubwa .
Aidha Dokta Ndumbaro amewataka kwenda vijijini kushughulikia kesi za Ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto jambo ambalo limekua linagharimu maisha ya makundi hayo.
Anasema ukatili wa kijinsia upo kwa sehemu kubwa vijijini huku wananchi wakikosa usaidizi wa kisheria hivyo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka inawajibu wa kutekeleza jambo hilo.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Ofisi ya Taifa Mashtaka Bw.Joseph Pande amewataka waajiriwa hao wapya kujiepusha na vitendo vya Rushwa kazini .
Amesema wafanyakazi wa serikali wanapaswa kufuata miongozi ya utumishi ikiwemo kuepuka vitendo vya rushwa,
Anasema Rushwa imekuwa ikiwanyima haki Wananchi wengine hasa wanyonge hivyo kutenda haki kwao kitawasaidia wananchi hao kupata haki yao bila kudhurumiwa.