Habari za Mastaa

Mapokezi ya Diamond Platnumz July 30 Dar es salaam.

on

30dmndNi mamia ya wakazi na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walioamua kwenda kumpokea Diamond Platnumz baada ya safari yake ya kutoka Marekani ambayo imekua njema kwa Tanzania baada ya kurudi na tuzo.

Mapokezi yalianzia  uwanja wa Julius Nyerere International Airpot kisha msafara ukaelekea mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ukipitia Buguruni,Kariakoo na baadae kumalizia nyumbani kwake Sinza.

20dmndWakati akiwa kwenye gari ya wazi Diamond Platnumz muda wote alikua kaishikilia tuzo yake aliyoipata Marekani kwenye tuzo za AFRIMMA ambapo kwa upande wake ameibuka na ushindi wa tuzo ya Msanii bora wa Afrika Mashariki.

Ratiba ya Diamond kuingia Tanzania ilikua iwe jioni ya Jana July 29 lakini kutokana na sababu walizosema zilizokuwa nje ya uwezo wao safari yao ikasogezwa mpaka leo July 30 na alifanikiwa kuingia saa 1 asubuhi.

Ingawa hali ya hewa ilikua imetawaliwa na manyunyu pamoja mvua ndogo ndogo,Hizi ni baadhi ya picha za mashabiki waliojitokeza kumpokea Diamond.

35dmnd

34dmnd

33dmnd

27dmnd

26dmnd

22dmnd

18dmnd

17dmnd

16dmnd

15dmnd

14dmnd

12dmnd

11dmnd

9dmnd

8dmnd

7dmnd

4dmnd

3dmnd

2dmnd

Tupia Comments