Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

DMX kwenye headlines, ajikuta matatani baada ya hukumu hii kutolewa Mahakamani!

on

DMX1

Headlines kwenye kurasa za burudani siku ya leo zinaandikwa na rappa maarufu kutoka Marekani, DMX.

Mwanzoni kulikua na kesi inayomhusu DMX kukwepa majukumu ya kumtumia aliyekuwa mke wake hela ya matunzo ya mtoto wao, DMX akapewa onyo na kuambiwa awe analipa hela hiyo, akakubali.

DMX2

DMX na mwanae

Kesi imerudi tena Mahakamani, gharama za hela zote alizokuwa anakwepa kulipa matunzo ya mwanae sasa  imefika dola 400,000 sawa na Mil. 800 za Kitanzania. Mahakama imetoa maamuzi na imesema jamaa atatumikia adhabu ya miezi sita jela kwenye Erie County Holding Center.

<> at J&R Music and Computer World on August 23, 2012 in New York City.

Licha ya hayo msanii huyu anashitakiwa kwa makosa mengine madogo, mwezi wa nne mwaka huu DMX na bodyguard wake walishitakiwa kwa kosa la kupora na kuiba kwa kutumia silaha ambako walimuibia mtu dola 3,200  sawa na Mil 6,400,000 za Kitanzania jijini New Jersey, kosa ambalo bado analikataa.

>>>“Sikumbuki kama nilishawahi kufanya kitu kama hicho mwezi wa nne, ndio tulikuwa New Jersey na nakumbuka tu kusimama Petrol Station na kuweka mafuta kwenye gari langu, hicho kitu mimi sijawahi kufanya, na kwa nini nifanye, shetani kila siku ananiandama ila I am special to God”. >>> DMX.

Nimekusogezea kipande hiki cha video kinacho ongelea hukumu yake.


Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments