Top Stories

Mitandao yamcheka Mgombea urais Marekani Donald Trump kwa kutoitamka vizuri Tanzania (+video)

on

Mgombea Urais kupitia Republican Marekani Donald Trump anazo headlines nyingine za kushindwa kutamka vizuri neno Tanzania kwenye hotuba yake kuhusu mambo ya nje ya Marekani alipokua akizungumzia ugaidi wa balozi za Marekani Tanzania na Kenya kulipuliwa.

Kibongobongo inawezekana tusingemcheka kwa jinsi alivyoitamka ila kwa wenzetu Marekani na Ulaya naona imekua ishu, vyombo vya habari vimeripoti kuhusu kushindwa huko kuitamka vizuri Tanzania kwenye hotuba yake ya kwanza ya mambo ya nje ambapo watu wamemkejeli na kumcheka, tazama hii video hapa chini…alivyotamka Tanz-eniya

Ukitazama kwenye hii video fupi hapa chini msemaji wa Ikulu ya Marekani alionekana akimcheka Trump kwa kushindwa kutamka neno Tanzania na hata hivyo kusema kifaa cha kumuongoza kusoma hotuba hakikuonyesha Tanzania inatakiwa kutamkwa vipi.


ULIIKOSA YA WASTARA KUELEZA KWANINI NDOA YAKE IMEVUNJIKA NDANI YA SIKU 80? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments