Mix

VIDEO: Jamaa wa Usalama walivyomdaka aliyetaka kumrukia mgombea Urais Donald Trump Marekani

on

Homa na mitetemo ya hasira kwa Wananchi wanaofatilia siasa hasa kwenye chaguzi kuu za nchi huwa ipo kila tukio hili kubwa linapofanyika, kuona watu wamepigana, kutoa lugha nzito au kuonyesha hisia zao za kumpinga mgombea flani moja kwa moja ni vitu vinavyotokea kwenye chaguzi kuu.

Washington 2

Mgombea Urais kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani Donald Trump alikoswakoswa kushambuliwa na mmoja wa Wananchi waliokusanyika kumsikiliza kwenye mkutano wake wa kampeni huko Ohio ambapo wakati jamaa huyo aliporuka uzio ili kwenda kumfata Trump jukwaani, walinzi walimdaka mapema hivyo hakufika kwenye jukwaa.

Polisi walimkamata huyo jamaa aitwae Thomas Dimassimo (22) lakini aliachiwa saa kadhaa baadae, unaweza kutazama hii video hapa chini kuona ilivyokuwa…

https://www.youtube.com/watch?v=UMmRaaATOxA

VIDEO NYINGINE NI HII HAPA CHINI…

https://www.youtube.com/watch?v=am_N6uJ08zk

Thomas Dimassimo aliendelea kuandika matusi kwa Trump baada ya kuchiwa kwa dhamani siku ya tukio na kukanusha pia kwamba alikua anakwenda kumshambulia kwa kisu jukwaani, alisema hakuwa na silaha yoyote ya kumdhuru Trump.

washington 3

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments