Muungano wa Asasi zinazojihusisha na masuala mbalimbali yanayowahusu Vijana Tanzania, Tanzania Youth Vision Association ‘TYVA’ umeeleza kuwa hadi kufikia 2030 idadi ya vijana duniani itafikia 18% huku Bara la Afrika likiwa na ongezeko la 42% ifikapo mwaka huo.
Aidha, Afrika imetajwa kuwa kinara wa kuwa na idadi kuwa ya vijana wenye umri mdogo zaidi duniani ikikadiriwa kuwa na watu 200 milioni wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24.
Tanzania inakadiriwa kuwa nchi ya kumi yenye idadi kubwa ya vijana duniani ikiwa na watu 22 milioni wenye umri wa chini ya miaka 25 ambao ni sawa na 47% kati yao wakiwa chini ya miaka 15 ambapo miaka kidhaa ijayo watafikia umri wa ujana.
Mtanzania aliyewahi kuweka rehani gari lake kumsadia kijana ada ya Shule!!!