Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde kwa kushirikiana na taasisi ya Bilal muslim mission of Tanzania ameamua kutoa huduma ya upimaji wa macho na kutoa matibabu yake ikiwemo upasuaji bure bila malipo kwa wananchi wake wa Dodoma kwa siku tatu mfululizo yaani kuanzia December 9 hadi 12 2016
Mavunde amesema…>>>’Kwakutambua matatizo makubwa ya macho kwa mkoa wa Dodoma ofisi ya bunge kwa kushirikiana na taasisi ya Bilal muslim mission of Tanzania leo tumeweka kambi ya siku tatau bure kwa lengo la kuwahudumia wananchi wote wenye uhitaji wa huduma za macho‘
‘Tunajua kuwa gharama za matibabu ya macho ni ghari hivyo tumeamua kuwahudumia wananchi wetu bila malipo yoyote kuanzia upimaji, kugawa miwani na hata wale wanaohitaji kufanyiwa upasuaji nao tutawahudumia pasipo malipo yoyote‘ –Anthony Mavunde
‘Tayari tumeweka utaratibu wa kuwapeleka wagonjwa wanaohitaji kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya mkoa na tunahakikisha hadi mgonjwa atakapokuwa amepona huku tukimgharamia huduma zote hadi chakula‘ –Anthony Mavunde
‘Lengo kuu ni kuwahudumia wagonjwa wasiokuwa na uwezo na huu ni utaratibu utakaokuwa ukifanyika kila mwaka katika mkoa wetu napia tunampango wa kushughulika na magonjwa yote kwa baadae ingawa kwa sasa tumeona tuanze na hili la macho kisha hatua nyingine zitafuata‘ –Anthony Mavunde
‘Kama mambo hayafanyiki mwambieni Rais siwafai aniondoe’ -RC Dodoma