Inatoka bunge Dodoma ambapo leo January 21 2017 Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu Ubunge iliyotoka kwa aliyekuwa Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge, kazi, ajira na watu wenye uemavu Dr. Abdallah Possi ambaye ameteuliwa na Rais kuwa balozi.
Taarifa ya spika imeeleza hizi >>> ‘Spika wa bunge Job Ndugai anapenda kuwataarifu Wabunge wote na wananchi kwa ujumla kuwa jana January 20, 2017 amepokea barua ya kujiuzulu ubunge iliyowasilishwa kwake na Dr Abdallah Possi‘
‘Kufuatia barua hiyo iliyozingatia masharti ya katiba ya mwaka 1977 ibara 67 (1) (g) ikisomwa pamoja na ibara ya 149 (1) (d), spika wa bunge amemwandikia rasmi Rais kuwa hivi sasa wabunge wa kuteuliwa na Rais waliopo bungeni ni saba hivyo nafasi zilizo wazi ni tatu baada ya Dr. Possi kujiuzulu‘
ULIPITWA? Sheria inasemaje pale Rais anapoapishiwa nje ya nchi kama wa Gambia?