Rais mteule wa Marekani Donald Trump alipongeza kuachiliwa kwa mateka na makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas siku ya Jumatano, yaliyokubaliwa siku tano tu kabla ya kurejea madarakani.
“Tuna mpango kwa ajili ya mateka katika Mashariki ya Kati.
Wataachiliwa hivi karibuni. Asante!” Trump alisema kwenye mtandao wake wa TruthSocial kabla ya kuwepo tangazo lolote rasmi kutoka kwenye Ikulu ya Rais anayeondoka madarakani Joe Biden.
Katika chapisho lingine la Truth Social Trump alidai kuthaminiwa kikamilifu kwa makubaliano hayo, akisema, “Makubaliano haya ya EPIC ya kusitisha mapigano yangeweza tu kutokea kama matokeo ya Ushindi wetu wa Kihistoria mnamo Novemba.”
Naamini dhamira ya serikali yake ya kutafuta amani na mazungumzo ya mikataba imetuma ishara yenye nguvu kwa ulimwengu.
Makubaliano hayo yanatarajiwa kuhusisha usitishaji vita kwa awamu, huku Hamas ikiwaachilia mateka 33 kati ya takriban 100 ndani ya Gaza wakati wa awamu ya awali ya siku 42.
Mjumbe maalum wa Trump katika eneo la Mashariki ya Kati, Steve Witkoff, alichangia pakubwa katika mazungumzo ya makubaliano hayo, akifanya kazi kwa karibu na wapatanishi wa Rais Biden.
Trump alimshukuru Witkoff na kuapa kwamba Marekani itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Israel na washirika wake ili kuhakikisha Gaza haiwi tena kimbilio salama la magaidi.
Aliandika, “tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na Israel na Washirika wetu ili kuhakikisha Gaza HAITAKUWA tena mahali salama pa magaidi.”