Top Stories

Donald Trump kaanzisha mtandao wake

on

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza rasmi kuwa hivi karibuni atazindua Mtandao wake wa Kijamii ambao utakuja kuwa Mtandao bora Duniani ambapo amefanya hivi kufuatia kufungiwa kutumia Facebook na Twitter baada ya kudaiwa kuchochea vurugu katika Majengo ya Bunge Marekani January 6 2021.

Mtandao huo utaitwa TRUTH Social na utamilikiwa na Trump Media & Technology Group (TMTG) na unatarajiwa kuzinduliwa mwezi ujao ambapo kwa sasa tayari upo tayari Apple Store wameanza kuuweka hewani kwa baadhi ya Watu kwa Pre – order.


Trump amesema “nimeamua kuanzisha TRUTH Social ili kupiga vita uonevu kwa wanaomiliki Mitandao, tunaishi kwenye Dunia ambayo Taliban wanatumia Twitter halafu Rais kipenzi cha Watu wa Marekani ananyamazishwa hii haiwezekani”

MTANZANIA ALIYEUAWA MAREKANI, FAMILIA YASIMULIA “ALIGONGA GARI KWA NYUMA”

 

Soma na hizi

Tupia Comments