Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataitaka benki kuu ya nchi hiyo kupunguza viwango vya riba pindi bei ya mafuta ghafi itakaposhuka.
Trump alisema, “Ningependa kuona bei ya mafuta ikishuka, na wakati nishati itapungua, hiyo itaondoa mfumuko wa bei.
Rais wa Marekani alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House siku ya Alhamisi na kusema hiyo itapunguza viwango vya riba moja kwa moja.”
Alisema bei ya chini ya mafuta itafanya kila kitu kuwa nafuu, na kupunguza viwango ni njia ya kutambua hili.
Mapema siku hiyo, Trump alijitokeza mtandaoni kwenye Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos, Uswizi.
Katika hotuba yake alisema ataomba Saudi Arabia na wanachama wa OPEC kupunguza gharama ya mafuta.
Trump pia alitoa wito wa kuleta viwanda nchini Marekani, akisema, “Njoo utengeneze bidhaa yako Amerika, na tutakupa kati ya kodi ya chini zaidi ya taifa lolote duniani.”