Michezo

DoneDEAL: GSM yamrudisha Niyonzima Yanga SC

on

Kiungo wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima amerejea rasmi Yanga SC clakitokea AS Kigali ya nchinikwao Rwanda, Haruna amecheza soka Tanzania kwa miaka nane mfululizo (2011-2019) na sasa anarejea rasmi tena Tanzania.

Haruna anarejea Yanga ikiwa ni miaka miwili imepita toka aondokea katika club hiyo na kujiunga na vijana wa Msimbazi Simba SC, kabla ya kumaliza mkataba wake 2019 na kuamua kurudi nchini kwao Rwanda katika club ya AS Kigali.

Kwa mara ya kwanza Haruna kuja Tanzania kucheza soka ilikuwa 2011 alipokuja kujiunga na Yanga SC akitokea APR ya Rwanda, baada ya kukaa Yanga kwa miaka sita, 2017 alijiunga na Simba SC na kukaa kwa misimu miwili kabla ya 2019 kuamua kurudi kwao Rwanda katika club ya AS Kigali.

AUDIO: Haruna Niyonzima anarudi Yanga? Bumbuli katoa jibu hili

Soma na hizi

Tupia Comments