Beki wa zamani wa Chelsea Branislav Ivanović ,36, raia wa Serbia amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea West Brom ya England.
Branislav Ivanović amejiunga na West Brom baada ya kuichezea Zenit Saint Petersburg ya Urusi kwa kipindi cha miaka 3 (2017-2020).
Ivanovic anarejea tena England hiyo ni baada ya kudumu na Chelsea kwa miaka 9 (2008-2017) huku akiripotiwa kuichezea zaidi ya michezo 260 na kufunga magoli zaidi ya 20.