Michezo

DoneDEAL: Mtanzania asaini Ligi daraja la tatu Ujerumani

on

Mtanzania Emily Mugeta ambaye amewahi kuichezea timu ya taifa ya Tanzania ya vijana ya U-17 amesajiliwa na club ya Freiburg FC ya Ligi daraja la tatu Ujerumani (Oberliga) kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mugeta amesaini mkataba huo akitokea SV Endigen ya Ligi daraja la nne nchini Ujerumani, hata hivyo mkataba aliosaini Mugeta utamuwezesha kuendeleza kituo chake cha kukuzia vipaji kilichopa Mwanza Ukerewe Mugeta Soccer Academy.

Emily Mugeta kutokana na kiwango chake alichokionesha ameendelea kupanda kiwango siku hadi siku na kupata timu ya madaraja ya juu kila leo, kutoka daraja la tano na nne na sasa la tatu.

VIDEO: KIMENUKA YANGA, MORISSON KASUSA AKIMBIA NJE UWANJANI “ACHA MASHABIKI WANIPIGE”

Soma na hizi

Tupia Comments