Michezo

DoneDEAL: Samatta atambulishwa Fenerbahce

on

Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na club ya Fenerbahce ya Uturuki akitokea Aston Villa ya England kwa mkataba wa miaka minne.

Fenerbahce wamempa jezi namba 12 Mbwana Samatta ambaye anaenda kuongeza nguvu katika kikosi hicho, club hiyo imewahi kumuwania mara kadhaa hata kabla ya kwenda Aston Villa lakini ndoto ya Samatta ilikuwa ni kucheza EPL.

Samatta anaondoka Aston Villa baada ya nafasi yake ya kucheza kuwafinyu sababu Aston Villa wamesajili wachezaji wengine wawili wa nafasi ya ushambuliaji Watkins na Traore, pamoja na Samatta nafasi hiyo ingekuwa na jumla ya wachezaji wanne.

 

Soma na hizi

Tupia Comments