Michezo

DoneDEAL: Simba SC imemrudisha kundini Kichuya

on

Club ya Simba SC leo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, imetangaza rasmi kumsajili mchezaji wake wa zamani Shiza Ramadhani Kichuya ambaye awali alienda kucheza soka nchini Misri katika club ya ENPPI.

Kichuya nchini Misri katika club ya ENPPI alikuwa kajiunga nayo kwa mkopo baada ya kuuondoka Simba kwenda Pharco FC ya Misri iliyokuwa imemsajili na kumtoa kwa mkopo moja kwa moja ENPPI ila leo Simba imemsajili katika mkataba ambo hawajaweka wazi muda wake.

Hata hivyo jaribio la Shiza Kichuya kwenda kucheza soka la kulipwa Misri halikuwa na mafanikio yoyote, kwani liliishia kupoteza nafasi yake ya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

AUDIO: DR Kigwangalla ahoji bilioni 4 za MO Dewji Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments