Michezo

DoneDEAL: Suarez anahamia Atletico Madrid

on

Club za FC Barcelona na Atletico Madrid zote leo zimetangaza muda huu kuafikiana juu ya uhamisho wa mchezaji Luis Suarez kuwa sasa anahamia Atletico Madrid kwa kiasi kinachotajwa kufikia euro milioni 6.

Wakati wowote kuanzia sasa baada ya Luis Suarez kupima vipimo vya afya atatangazwa kuwa mchezaji rasmi wa Atletico Madrid, hiyo ni baada ya kuwa nje ya mipango ya kocha mpya wa Barcelona Ronald Koeman.

Kabla ya uhamisho huo Suarez baada ya kuthibitika kuwa anaondoka Barcelona, chaguo lake la kwanza lilikuwa ni kwenda kucheza soka Italia katika club ya Juventus ila kutokuwa mchezaji anayetoka nchi za umoja wa Ulaya (EU) na kushindikana kupata uraia kumekwamisha dili hilo.

Soma na hizi

Tupia Comments