Habari za Mastaa

Majibu ya Diamond Platnumz >> kilichomtoa machozi? Kazi na Wema? hakwenda kwa Zari Uganda.. (+Audio)

on

Staa wa Bongofleva, Diamond Platnumz amerudi kwa uzito mkubwa kwenye headlines za muziki baada ya kuachia ngoma ya ‘Utanipenda’.

Baada ya kuachia video ya ngoma hiyo, leo December 21 2015 kaachia audio rasmi hewani kwenye show ya ‘Leo TenaClouds FM… kwenye stori zilizopigwa aliulizwa pia kuhusu sababu iliyofanya apost kipande cha video kilichomtoa machozi wakati mama yake anaigiza.

DIAMOND II

Ile stori ya video nimeandika mimi… wakati wanashoot nilikuwa nawaelekeza kwamba inabidi iweje… alivyoanza kuigiza nikajikuta nashindwa kuvumilia, nikahama. Hata yeye mwenyewe hisia zilimgusa, ukiangalia kwenye video utafikiri anataka kulia kweli, nilijisikia vibaya.. sijawahi kumuona mama yangu anaigiza… Wakati naangalia video kwa mara kwanza nilitokwa machozi, japo naona kama nimeizoea ila nikikaa pekeyangu naangalia, naona kama ni kweli hivi.‘>>> Diamond Platnumz.

DIAMOND VI

Kwenye video ya ‘Utanipenda‘, ameonekana pia mrembo Jackline Wolper, sababu ya Wolper kuonekana ni hii hapa >>> Wolper tunaheshimiana, tuna uhusiano mzuri wa kikazi na kiundugu… katika mastaa wenye nguvu, Wolper lazima umtaje..

Diamond Platnumz na Jackline Wolper

Diamond Platnumz na Jackline Wolper

Kuna ukweli wowote kwamba nafasi ya Wolper ilikuwa acheze Wema Sepetu na akakataa? Majibu ni haya >>> ‘Sio kweli, sijawahi hata kuwaza hivyo… hapo katikati kulikuwa na stori kwamba mimi natumia nyota yake, kwa hiyo nisingeweza kumshirikisha katika kazi yangu yoyote hata kama ni biashara ambayo ingempa pesa, ingeonekana nimetumia nyota yake… Huwezi kuona kazi yangu au changu chochote kinahusiana na Wema kabisa.. Mimi nina timu, natumia nguvu nyingi kuifanya kazi yangu, ikionekana unatumia nyota ya mtu ni kama unaitukanisha.’>>> Diamond Platnumz.

Diamond amesema alikuwa Uganda kwenye show yake ambayo ilifanya poa sana, lakini kwa sababu alikuwa na mkataba wa show yake, alijikuta akishindwa kuhudhuria show ya Zari All White Party.

Sauti ya Interview yote hii hapa mtu wangu, Diamond Platnumz na stori zote kwenye ‘Leo Tena‘.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments