Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Yanga SC wamempa sababu Haji Manara ya kujigamba leo

on

Mashabiki wa Simba SC wakiongozwa na msemaji wao Haji Manara katika mitandao ya kijamii wameendelea kufurahia na kujitamba kuhusiana na matumaini makubwa ya kutetea taji lao la Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019, hiyo ni baada ya watani zao wa jadi Yanga kupoteza point 2 leo mjini Mtwara katika mchezo dhidi ya Ndanda FC.

Yanga SC leo walikuwa Mtwara walikosafiri na kikosi chao cha wachezaji 20 lakini katika mchezo wao wa 29 wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda FC, wamejikuta wakipoteza point mbili baada ya kulazimishwa sare ya kufungana goli 1-1, Ndanda ndio walianza kupata goli dakika ya 20 ya mchezo kupitia kwa Mayanga ila Yanga wakasawazisha goli dakika ya 62 kupitia kwa Papy Tshitshimbi.

Game hiyo imemalizika kwa timu hizo kugawana point moja moja, ila hiyo ni furaha kwa Simba SC kwa sababu wana viporo 7 ili kufikia michezo 29 ya Yanga ila Simba wanafurahia kutokana wanaamini kuwa hata iweje hawawezi kuruhusu timu yao ipoteze michezo yote saba ya viporo kirahisi na kuwafanya Yanga watwae taji hilo, hiyo ndio sababu inayowafanya mashabiki wa Simba na afisa habari wao wawe na furaha.

Yanga kwa sasa wanaongoza kwa kuwa na point 68 wakicheza michezo 29 sawa na Azam FC waliopo nafasi ya pili kwa kuwa na point 62 ila Simba SC wapo nafasi ya tatu kwa kuwa na point 57 ila wamecheza michezo 22 na wamebakia na viporo saba kutokana na ratiba yao kuingiliana na ratiba ya michuano ya CAF Champions League wanayoshiriki wakati huu wakiwa robo fainali na mchezo wao mmoja dhidi ya JKT Tanzania jana April 3 uliahirishwa kutokana na uwanja wa Jamhuri kujaa maji.

Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….

Soma na hizi

Tupia Comments