Habari za Mastaa

Drake aelezea kufanana kwa wimbo wake wa ‘Hotline Bling’ na ‘Cha Cha’ wa D.R.A.M..!

on

Kumekuwa na maneno mengi baada ya Drake kuachia video ya wimbo wa Hotline Bling, licha ya mashabiki wengi kuipenda video ya msanii huyo wapo pia waliojitokeza kusema kuwa Drake kaiba beat ya wimbo wa Cha Cha wa msanii mwengine Marekani mwenye jina D.R.A.M… sawa, ila Drake anaichukuliaje hii?

Kwenye interview aliofanya na jarida la Fader, Marekani, Drake aliulizwa kuhusu kufanana kwa beat ya Hotline Bling na ile ya Cha Cha ya kwake D.R.A.M… kwenye kupiga stori na msanii huyo, Drake alikuwa na haya ya kusema…

1112

>>> ” Unajua, ukienda Jamaica utakutana na mionoko ya ‘dancehall riddim’, na ukisha isikia miondoko hiyo basi utakutana na watu tofauti watakaopenda kufanya nyimbo zao kwa miondoko inayofanana na hiyo pia. Sasa vuta picha hiyo kwenye muziki wa Rap, au muziki wa R&B. Vuta picha kama wote tungekuwa na beat moja na kila mtu -me, wewe, na yule na wale – wote inatubidi tutengeneze ngoma kali kwa kutumia mfano wa beat hiyo…”

HLB CHACHA

>>> “Nadhani hata ingekuwa ni mimi, ningechagua beat ambayo kidogo ina miondoko kama hiyo, miondoko ya kuchangamsha, ambapo kwako na kwa watu wengine mgetumia neno ambalo ni common kwenu ‘kuiga/kuiba’… ila kwangu mimi ni kujaribu kufanya kitu chenye miondoko ile sema kwenye Rap so Hotline Bling ikawa hivyo. Na nimeupenda wimbo kusema kweli…” <<< Drake.

Nimeisogeza kwako video ya Drake na D.R.A.M hapa chini unaweza kuzicheki kuona kama kweli zinafanana miondoko na beats.

  1. D.R.A.M – Cha Cha.

2. Drake – Hotline Bling.

 

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments