Habari za Mastaa

Ijue sababu ya Drake kufanya remix ya ‘Ojuelegba’ na mtazamo wa muziki wake Nigeria!

on

Msanii kutoka Nigeria, Wizkid alipata shavu kubwa sana kwenye headlines za entertainmnet Marekani baada ya superstaa kutoa Cash Money Records, Drake kuomba kufanya nae remix ya wimbo wake wa Ojuelegba miezi michache iliyopita.

Lakini ulishawahi kujiuliza hiyo collabo ilitokeaje tokeaje, na kwa nini Drake aliamua kufanya remix ya Ojuelegba na Wizkid?… Siku chache zilizopita Drake alifanya exclusive interview na gazeti moja la entertainment huko Marekani na kuelezea sababu zilizomsukuma yeye kufanya hivyo…

WIZKID

Wizkid.

>>> Nimekuwa nikimsikia sana Wizkid na najua anatokea Nigeria lakini pia najua muziki wa Nigeria unafanya vizuri sana Africa na kupitia muziki wao watu kama Wizkid wameweza kutengeneza jina kubwa nyumbani na hata sehemu mbalimbali duniani… na niliamua kufanya ile remix kwa sababu nilisukumwa kutoka moyoni na mwanzoni nilikuwa sifikiri sana kupeleka brand yangu Nigeria lakini baada ya ile remix kuwagusa mashabiki wengi kutoka Africa nimeona kuna kila sababu ya mimi kufikiria kollabo nyingne na mastaa kama Wizkid kutoka Nigeria…” <<< Drake

Hapa chini nimekuwekea remix ya Ojuelegba ya kwake Wizkid feat. Drake & Skepta.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments