Rapper kutoka kwenye lebo ya Cash Money Records, Drake anazidi kufaidi matunda yake mengi anayoyapata kupitia muziki wake kwa kuvunja rekodi kwenye chati mbalimbali za muziki.
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali zilizotolewa na Neilsen Soundscan, album ya Drake iliyopewa jina ‘If You’re Reading This It’s Too Late’, imetajwa kuwa Album yenye mauzo ya juu zaidi ya kidigital kwa mwaka huu wa 2015, ikiwa imeuza zaidi ya copy 951,000 za kidigital kufikia mwezi wa September 2015.
Album ya If You’re Reading This Its Too Late iliachiwa rasmi tarehe 21 February 2015 kwenye mitandao ya kidigital na ndani ya wiki ya kwanza tu ya mauzo, Album hiyo iliuza idadi ya copy 535,000, na ndani ya wiki ya kadhaa ya mauzo Album hiyo ikashika #1 kwenye chati ya Billboard 200.
Ukiacha mauzo ya kidigital peke yake, album hiyo ilipoingia madukani iliuza copy nyingi zaidi za CD ukichanganya na idadi ya mauzo ya kustream online pia, kitendo hiki kilisababisha Album hiyo kupata platinum status, ndani ya miezi michache tu ya kuwa sokoni!
Big Up sana kwa mtu wetu Drake!
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.