Habari za Mastaa

Kama asingekuwa msanii wa HipHop, unajua Drake angekuwa nani leo?

on

Rapper kutoka lebo  ya Cash Money Records, Drake ni msanii wa vipaji vingi sana… kwanza ana uwezo wa kuimba na kurap kwa wakati mmoja, lakini kitu kingine kuhusu yeye ambacho nilikuwa sikijui ni kwamba Drake pia ni muigizaji mzuri sana!

Nimekutana na interview ya Drake aliyofanya na jarida la W Magazine, la Marekani na miongoni wa vitu alivyoviongelea msanii huyo ni hamu yake kubwa kurudi kwenye industry ya uigzaji kwa sababu kabla ya kuingia mazima kwenye game ya muziki Drake alishawahi kupata fursa ya kuigiza kwenye movie moja iliyopewa jina “Degrassi: The Next Generation” alivyokuwa mtoto.

W ART

Drake: (Cover W Magazine)

>>> “Nina hamu kubwa sana kurudi kwenye uigizaji. Hakuna anaeniuliza kama napenda kuigiza movies, na licha ya kwamba muziki ndio uwanja wangu mkubwa sasa hivi, ningependa pia kuigiza movie. Hayo ndio maisha niliyoishi mwanzoni, na itakuwa fursa nzuri kuishi maisha hayo kwa mara nyingine…” <<< Drake.

W ART 2

Drake; (W Magazine Photo Shoot).

Alipoulizwa kwanini aliacha kuigiza alivyokuwa mtoto Drake alisema…

>>>“Baada ya muda waligundua kuwa nilikuwa najihusisha na fani mbili (uigizaji na muziki) kwahiyo wakanambia nichague kitu kimoja kati ya hivyo viwiliNikachagua muziki lakini kama nisingekuwa msanii wa muziki wa rap leo basi naamini ningekuwa muigizaji wa movie.” <<< Drake.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments