Pamoja na kuwepo kwa kampeni za kuzuia watoto kutumikishwa kwenye shughuli zozote ambazo ni hatari kwa maisha yao, ripoti mpya ya SKY NEWS imeonesha kuwa watoto wadogo mpaka wa miaka minne wanatumikishwa kufanya kazi ya uchimbaji madini huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Uchunguzi uliofanywa na Sky News umeonesha kuwa wengi wa watoto wanaofanya kazi kwenye machimbo ya madini Congo DRC hawana wazazi na wengine ni waathirika wa vita za wenyewe wa wenyewe waliokosa makazi, hivyo kuamua kufanya kazi kwaajili ya kupata riziki.
Dorsen mwenye miaka 8 na rafiki yake Richard wamezungumzia mazingira ya kazi hiyo ya uchimbaji. >>>Mimi hapa natumika, mama yangu alishafariki, kichwa mgongo unaniuma na mbavu, huwa wanatusukuma tunaenda kufanya kazi kila siku<<< – Dorsen na Richard
Kutana na watoto wanaotumiwa katika uchimbaji madini ya kutengeneza simu nchini Congo, Dorsen miaka 8 na Richard '11' wanaeleza kila kitu pic.twitter.com/LhjUl8qfYK
— millardayo (@millardayo) February 27, 2017
VIDEO: Walivyookolewa wachimbaji 15 waliofukiwa mgodini Geita, Bonyeza play kutazama