Habari za Mastaa

Baada ya ‘Straight Outta Compton’, Dr. Dre sasa hivi anafikiria kufanya nini?

on

Baada ya kuweka headlines nyingi na movie  ya ‘Straight Outta Compton’, Dr. Dre amekuwa akifikiria vitu vingi sana, je Dr. Dre ana mipango gani kimuziki sasa hivi? Kama wewe ni shabiki wa producer huyo basi hii taarifa ikufikie popote pale ulipo…

Kwenye kipindi chake cha The Pharmacy kinachoruka kupitia Beats 1 Radio, Dr. Dre alipata time ya kufanya interview na rapper Snoop Dogg na kumuelezea mawazo yake machache kuhusiana na kurudi jukwani na Snoop Dogg mwenyewe, Eminem pamoja na Kendrick Lamar, na kwenye safari yake yote ya muziki Dr. Dre anadai hajawahi kufanya tour kubwa Europe!

DRE4

Dr. Dre.

Licha ya yeye kuwa na nia hiyo, safari hii producer huyo amesema angependa kuonyesha upendo kwa mashabiki wake wa Europe kwa kufanya tour hiyo na mastaa watatu wakubwa katika game ya muziki wa HipHop na kuperform nao huko kwenye jukwaa moja…

>>> “nataka niite hiyo tour ‘Beats & Rhymes’. Nataka niwepo mimi, wewe, nataka pia awepo Eminem na Kendrick Lamar… yeah ningependa kufanya tour Europe nzima na kuiita Beats & Rhymes, kuchukua coverage na production ya tour nzima kutoka hapa mpaka huko na kuwaonyesha mashabiki wangu wa Europe upendo wa kipekee sana kwa sababu wamekuwa na mimi kwa miaka mingi na upendo wao umekuwa wa kipekee sana kwangu kwenye safari yangu ya muziki… So hiyo ndio ndoto yangu kwa sasa. Natumaini tutaifanikisha.” <<< Dr. Dre.

DRE3

Snoop Dogg.

Wakati Dr. Dre anaongea yote haya, Snoop Dogg alionekana kumuunga mkono producer huyo bila kipingamizi… na pia kutoa wazo la jina lingine la tour hiyo…

>>> ” Hiyo ndoto imekaa vizuri… mimi ningeshauri tuiite ‘Hoodstock’ au vipi?” <<< alisema Snoop Dogg.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments