Habari za Mastaa

Dr. Dre kwenye headlines, kufikishwa mahakamani na mfanyakazi wake wa ndani!

on

Rapper na producer maarufu Marekani, Dr. Dre ameiingia kwenye headlines baada ya mtandao wa The NewYork Daily News kuripoti kuwa mfanyakazi wa Dr. Dre mwenye jina Raquel Sagustume kufikisha Mahakamani malalamiko yake ya kuteswa akiwa anafanya kazi nyumbani kwa producer huyo.

DR2

Kwa mujibu wa maelezo ya dada huyo Raquel Sagustume, anadai kuwa alikuwa anaonewa na wafanyakazi wengine ikiwemo na binamu wawili wa Dr. Dre. Mtandao wa The NewYork Daily News umeripoti..

>>> “Sagustume amesema wafanyakazi wengine – binamu wawili wa kike – walitishwa na uwezo wake wa kazi na badaae kuanza kumtuma kinyume na haki  zake za kazi ili awafanyie kazi zao, kitendo kilichosababisha apate matatizo ya mwili…” <<< nukuu kutoka kwa mtandao wa The NewYork Daily News.

DR3

Licha ya kupokea zaidi ya $ 1,870 kwa wiki ambayo ni zaidi ya milion 4 za Tanzania kwa wiki, mfanyakazi huyo amelalamika kuwa Dr. Dre pia alikuwa hamlipi hela ya overtime ya muda wote aliyokuwa anafanya kazi nyumbani kwake, kitu kilichoababisha asiweze kufurahia likizo yake vizuri! Ameongezea kuwa alipatata mshituko wa moyo uliyosababishwa na yeye kuwa kwenye mazingira ya hofu na kuonewa.

DR1

Dr Dre na mke wake Nicole Young.

Kwenye kesi yake, Raquel Sagustue anaweka lawama kubwa kwa Dr. Dre na mke wake, Nicole Young kwa kutodhibiti vitendo vya uonevu kwenye nyumba yao. Raquel Sagustume amekuwa akifanya kazi kwa Dr. Dre kwa miezi 13 tu!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments