Michezo

VIDEO: Kaseja kashindikana kwa penati, cheki alivyodaka penati

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jumapili ya Septemba 8 2019 ilicheza mchezo wake wa marudiano wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya kupambania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar dhidi ya Burundi.

Tanzania ilicheza game hiyo na dakika 120 kumalizika kwa sare ya kufungana magoli 1-1, goli la Tanzania likifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 30 huku la Burundi likifungwa na Feiston dakika za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko, mikwaju ya penati ndio iliamua timu ipi isonge mbelee baada ya kuwa na aggregate ya 2-2.

Mikwaju ya penati Tanzania ikawa na bahati zaidi baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa penati 3-0, hivyo kuingia hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, Juma Kaseja ndio alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kucheza penati ya kwanza iliyoleta nguvu kwa Taifa Stars na kuwadhoofisha Burundi.

EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE

Soma na hizi

Tupia Comments