Top Stories

Drone ya Marekani yauwa familia ya watu tisa huko Afghanistan

on

Watu tisa wa familia moja wakiwemo Watoto sita wamefariki kwenye shambulio la roketi za Marekani zilizokua zimerushwa kulilenga gari lililokua na Mtu aliyekua anakwenda kufanya shambulizi la kujitoa muhanga Kabul, Afghanistan.

Gari hilo liligundulika na Jeshi la Marekani kuwa limembeba Mwanachama wa Kundi la ISIS ambae alikua anaendesha kwenda kujitoa muhanga kwenye uwanja wa ndege wa Kabul ambao Marekani imeweka Raia wake na Raia wa Afghanistan wanaosubiri kuhamishwa kwenda Marekani.

Mmoja wa Ndugu amesema “hawa waliouwawa walikua familia ya kawaida, na mwenye umri mdogo kabisa miongoni mwao ni Mtoto wa miaka miwili, hapa walikua wanakaa Kaka zangu na familia zao, idadi ya waliofariki inaweza kuwa kuwbwa hata 20 kwasababu kombora lilifika mpaka kwenye nyumba wanamoishi, wamekatika vipandevipande huwezi kutambua chochote”

Jeshi la Marekani limesema gari lililokua na Mtu huyo wa kujitoa muhanga lilikua na vilipuzi vingi ndio maana liliposhambuliwa mlipuko ulifika mpaka kwenye nyumba wanazoishi Watu.

WATU WAANGUKA KUTOKA KWENYE NGEGE ANGANI, MACHAFUKO AFGHANISTAN, TALIBAN WACHUKUA NCHI

 

Tupia Comments