Top Stories

Ahukumiwa kwa kumpiga mumewe kwa miaka 12

on

Japokuwa ni desturi mbaya na inayopingwa na wanaharakati wa masuala ya kijinsia, kwenye jamii nyingi hususani za Kiafrika, ni suala la kawaida kusikia wanaume wanapiga wanawake ambao wako nao kwenye ndoa au mahusiano ya kimapenzi.

Jambo hili limekua limekua tofauti huko Uingereza ambapo hivi karibuni Mahakama ya Hakimu Mkazi nchini humo imetoa hukumu kwa mwanamama Hellen Tweedy, 45, kufuatia tabia yake ya kumpiga mume wake Neil Tweedy, 45, mara kwa mara kwa miaka 12 tangu waoane kutokana na mitafaruku mbalimbali.

Imeelezwa kuwa mwanaume huyo alichoka na tabia hiyo ya mkewe na kuamua kutegesha kamera ndani ya nyumba yao kurekodi vitendo vya mwanamke huyo ili iwe kama ushahidi na baadaye kuifikisha video hiyo polisi kisha kufungua kesi ya vitendo vya ukatili. Mwanaume huyo hata hivyo amemtetea mkewe kwa kusema ni mwanamke mzuri na mchapakazi na huenda hufanya hivyo wa sababu ya stress za kazini kwake.

Ulipitwa na hii?BEEF LINGINE? Miss Kiki adai Rosa Ree anaiga, hana heshima

Hii je?IDRISS KAFUNGUKA!! Ni kuhusu Wanaume wanaolelewa na wanawake

Soma na hizi

Tupia Comments