Mix

Taarifa nyingine kuhusiana na mzigo mkubwa wa dawa za kulevya.

on

HeroineBado taarifa za watu kukamatwa na dawa za kulevya zimeendelea kuchukua nafasi, ni siku chache zimepita tangu Polisi wa Nigeria kumkamata mtu ambaye alikuwa anasafirisha dawa za kulevya akiwa amefisha ndani ya viatu vya kike ndani ya mabegi makubwa mawili, leo kuna watu wengine wane wamekamatwa wakisafirisha mzigo wa dawa hizo.

Polisi wa Mombasa, Kenya wamesema wanawashikilia watu wanne kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine.

AAskari wa Kenya wakiwa eneo walipowakamata watuhumiwa hao.

Askari Polisi wa Kenya.

Mpelelezi ambaye anafanya kazi na kikosi cha kuzuia Mihadarati, Kenya Anti-narcotics Unit, Hamis Masha amesema watu hao wanadaiwa kuhusika na mifuko 98 za dawa hizo zilizokamatwa Nairobi na walikuwa wakitafutwa na maafisa wa usalama wa Marekani wa DEA.

Maafisa hao wamesema dawa hizo huwa zinasafirishwa kutoka Pakistan na Iran na  kuingia katika bandari za Afrika Mashariki ambako kuna ukaguzi duni wa bidhaa zinazoingizwa na baadaye kupelekwa Ulaya.

Watu hao waliokamatwa wawili wana asili ya Kenya na wawili asili ya India.

Tupia Comments