Timu za Hispania zimepata mafanikio makubwa kwenye ligi ya Europa miaka ya hivi karibuni lakini msimu huu wanakutana na changamoto kutoka kwa timu za Ligi ya England, Arsenal pamoja na Chelsea ambazo zimefuzu kuingia hatua ya 16 bora, kwa misimu saba iliyopita, timu za LaLiga zimeshinda Kombe hilo mara tano.
Huku Sevilla wakishinda mara tatu mfululizo (2014, 2015 na 2016), wakati Atletico Madrid walishinda mwaka 2012 na 2018, timu pekee ambazo ziliingilia kati katika kipindi hicho ni Chelsea (2013) na Manchester United (2017), usiku wa leo zitachezwa mechi za kwanza za hatua ya 16 bora ambapo timu za Chelsea na Arsenal zinategemewa kufuzu kwenda hatua inayofata.
Chelsea watakuwa nyumbani dhidi ya Dynamo Kyiv, timu ambayo imeshiriki mara kwa muda mrefu sana katika mashindano makubwa ya Ulaya, wameshiriki mfululizo tangu msimu wa 1989/90, mahasimu wa Chelsea, Arsenal wana kocha ambaye anajua nini kinahitajika ili kushinda Kombe hilo. Unai Emery ambaye aliwaongoza Sevilla kushinda mara tatu mfululizo taji hilo.
‘Washika Bunduki’ watakuwa ugenini kwa Rennes kucheza mchezo wa kwanza – Naye kiungo wa timu hiyo Grani Xhaka alisema >>>“Ukishinda Europa League unaenda moja kwa moja kwenye Champions League. Bado naamini Premier League ni nafasi yetu nzuri kufikia Ligi ya mabingwa” Sevilla (vs Slavia Prague) na Valencia (vs Krasnodar) wataanza safari ya kuitafuta robo fainali wakiwa nyumbani huku Villarreal watasafiri takriban kilomita 4000 kuwafata Zenit St Petersburg.
Ligi ya Serie A inawakilishwa na Napoli pamoja na Inter Milan ambao nao wana nafasi ya kufanya vizuri. Napoli wanacheza dhidi ya Red Bull Salzburg huku Inter wakianzia ugenini kwa Frankfurt.
Mchezo wa Chelsea dhidi ya Dynamo Kyiv utachezwa saa 5:00 Usiku na ule Arsenal vs Stade de Rennais FC ni saa 2:55 Usiku. Zote mbili zitaonyeshwa Mubashara kupitia chaneli ya ST World Football.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake