Taasisi ya magonjwa ya moyo ya JKCI wameanzisha huduma mpya ya kuwapima mama wajawazito wa wiki 20 ili kugundua kama watoto wao wana magonjwa ya moyo ili waanze kupanga kuhusu matibabu yao ikiwemo kujiandaa kwa tiba ya upasuaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Prof Mohammed Janabi ameeleza kuwa mwaka jana walizaliwa watoto milioni 2, na kati yao watoto 20000 walizaliwa na magonjwa ya moyo na kuongeza kuwa asilimia 75 ya wanaofanyiwa upasuaji kwenye taasisi hiyo ni watoto wadogo.
Aliongeza kuwa mtu mmoja wa umri wowote akipelekwa India kufanyiwa upasuai wa moyo ina gharimu shilingi milioni 30 na hivyo kuna umuhimu wa kuanza kufanya uchunguzi kwa watoto kabla hata ya kuzaliwa ili kuwatibu mapema na kuepukana na gharama hizi lakini cha zaidi ni kulinda maisha yao.
Ulipitwa na hii? Kiwanda cha Matairi cha Superdol chateketea kwa moto