Mix

PICHA: Lilipoonekana Gari la Manji baada ya kuchukuliwa na Ambulance Polisi

on

Leo jioni February 12 2017 Mfanyabiashara maarufu Yusuph Manji kwenye kituo cha Polisi Kati Dar es salaam alionekana akichukuliwa na gari la Wagonjwa aina ya Land Cruiser ikiwa ni baada ya kuhojiwa na Polisi toka Alhamisi February 9.

Baada ya gari hilo kumchukua haikujulikana alikopelekwa lakini halikuondoka peke yake kituoni hapo, gari lililoongoza msafara huo lilikua gari aina ya Range Rover linalomilikiwa na Mwenyekiti huyo wa Yanga.

Taarifa ilizopata millardayo.com na AyoTV ni kwamba msafara huo ulikwenda moja kwa moja kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Muhimbili Dar es salaam ambako watu mbalimbali wanaosumbuliwa na moyo hupata matibabu.

Hii picha hapa chini ni gari hilo aina ya Range Rover likiwa nje ya Taasisi hiyo ya moyo ambapo millardayo.com na AyoTV zinaendelea kufatilia zaidi kujua kinachoendelea.

ULIPITWA? Maneno ya Yusuph Manji baada ya kutajwa na Mkuu wa mkoa Paul Makonda kwenye sakata la dawa za kulevya, tazama kwenye hii video hapa chini

VIDEO: Yusuph Manji alivyochukuliwa na gari la Wagonjwa kituo cha Polisi Kati Dar es salaam

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako Millard Ayo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID NA IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments