AyoTV

Mwendokasi Gerezani kusimama kwa dakika 180 kesho

on

Kama wewe ni mtumiaji wa Mabasi ya mwendokasi Dar es salaam hasa upande wa Kariakoo inabidi ujue kesho Jumatano January 25 Rais Magufuli anaweka baraka zake kwenye mradi huo hivyo safari za kuingia na kutoka zitasimama kwa muda.

Deus Buganywa kutoka UDART amesema ‘uzinduzi wa mradi utafanywa na Rais Magufuli na kutokana na shughuli hiyo kufanyika Mtaa wa Gerezani, tutasitisha kwa muda huduma za mabasi yanayotoka FIRE kuja GEREZANI kati ya saa 4 asubuhi mpaka saa 7

ULIPITWA? Kwa mara ya kwanza Mabasi ya Mwendokasi Dar es salaam, tazama hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments