Hivi kariburi Rais JPM alikabidhiwa ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma ambapo ilibainika watumishi 9,932 walighushi vyeti ili kupata ajira katika ofisi za umma.
Kutokana na ripoti hiyo ofisi kadhaa za umma katika jiji la Dar es Salaam zimekuwa zikishuhudia watumishi wakianza kuondoka.
Ayo TV na millardayo.com imemtafuta Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ambaye moja ya mambo aliyoyatolea ufafanuzi ni pamoja na athari za sakata hilo katika ofisi mbalimbali za jiji la Dar es Salaam na hapa anafafanua.
“Kweli suala hili lina changamoto yake. Tayari madhara makubwa yameanza kutokea. Kwa mfano mimi secretary wangu sasa hayupo. Na hata secretary wa Mkurugenzi hayupo.” – Isaya Mwita.
Nimekuewekea full video, bonyeza play kutazama…
VIDEO: JPM akabidhiwa Ripoti ya Uhakiki wa Vyeti vya Watumishi wa Umma – Dodoma. Bonyeza play kutazama…