Top Stories

Unamjua Mbunge aliyefunga ndoa Tz leo Novemba 22…?

on

weddingKwenye headlines za bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa pili wa mastaa wa bunge hilo imeongezeka hii nyingine leo Mbunge aliefunga ndoa.

Tumezoea Wabunge wetu wakipewa nafasi ya kuchangia jambo ndani ya kikao cha Bunge huwa wanaanza kwa pongezi, utasikia hivi; “.. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge au Waziri………

Jumatatu kikao cha Bunge kitaendelea na nadhani hautoshtuka ikitokea Mbunge hata mmoja akisema hivi; “… Nimpongeze sana Mheshimiwa David Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini kwa kufunga ndoa siku ya Jumamosi..”

Yes.. ni kweli.. mbunge huyo amefunga ndoa leo November 22 2014 Kigoma, ujumbe alioandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook ni huu hapa; “..Bwana Harusi David Kafulila akiwa na msimamizi wa ndoa yake Deo Filikunjombe na marafiki zake David Silinde na Mwami..” halafu kuna picha aliyoiweka akiwa na Wabunge hao.

Endelea kufuatilia millardayo.com kwa taarifa zaidi mtu wangu.

Zitto David KafulilaHautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments