Mix

Diamond azungumza kinachoendelea kati yake na Hamisa Mobetto

on

Mwimbaji wa Bongofleva kutoka WCB Diamond Platnumz amefunguka kuhusu story ambayo ilimake headline akidaiwa kuwa mapenzini na Hamisa Mobetto ambapo inadaiwa amempa ujauzito Mwanamitindo na kuonekana kuwa karibu na mama yake Diamond.

Diamond amezungumza kupitia kipindi cha XXL ya Clouds FM June 21, 2017 ambapo amesema hakuwai kuwa na uhusiano na Hamisa pia hafahamu lolote kuhusu ujauzito bali ni story anazozisikia tu:>>>“Kuhusu mimba ya Hamisa mimi sijawahi kuwa na mahusiano naye. Hizi ni stori ambazo kila siku hata mimi nazisikia.

“Toka nimefanya na Hamisa Mobetto video ya Salome watu wameongea kweli lakini mimi sina mahusiano naye.” – Diamond Platnumz.

VIDEO: Mchekeshaji Eric Omondi alivyovamia stage kucheza SALOME na Diamond

Soma na hizi

Tupia Comments