Top Stories

DStv yamwaga ofa kwa wateja wake sasa ni Promosheni ya ‘Panda Tukupandishe’

on

MultiChoice Tanzania imetangaza promosheni maalum kwa wateja wa DStv ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu itakuwa ikiwapandisha vifurushi wateja wake. 

Hii ni promosheni inayowawezesha wateja wa DStv wanaokidhi vigezo (wateja waliokatika, wateja wanaoendelea na wateja wapya) kupata fursa ya kulipia kifurushi kinachofuatia cha juu yake na kupandishwa kwa kupatiwa kifurushi cha juu ya kile walicholipia kwa muda maalum. 

Hii itategemea na kifurushi ambacho mteja alikuwa amelipia hadi kufikia tarehe 8 Januari 2021 au kifurushi alichojiunga nacho baada ya tarehe 8, Janurai 2021. Mathalan, Mteja wa kifurushi cha Bomba, akilipia kifurushi cha Family, atapandishwa hadi kifurushi cha Compact bila malipo ya ziada kwa mwezi mmoja.

“MultiChoice Tanzania inafurahi kuzindua rasmi promosheni yake maalum ya ‘Panda tukupandishe’ hii ikiwa ni njia mojawapo ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kuwa nasi na pia njia ya kuwahakikishia kuwa tumejipanga vema kuendelea kuwapatia burudani isiyo na kifani” amesema Ronald Shelukindo, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania wakati wa uzinduzi rasmi wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam.

Amesema kampuni hiyo inaendelea kuwapatia wateja wake burudani ya kina bila kusahau maudhui mengine kama Habari na elimu, huku ikihakikisha kuwa wateja wake wanapata maudhui kemkem na ya kusisimua ya ndani na nje.  

Kaimu meneja wa thamani kwa wateja Lucy Kisasa amesema kama zilivyo promosheni nyingine, kuna vigezo na masharti ambavyo vitafuatwa ili mteja aweze kunufaika na promosheni hii. Amesema promosheni hii ni kwa wateja wa DStv waliopo Tanzania, wale ambao akaunti zao ziko hai na wale ambao akaunti zao zimekatika. Pia inawahusu wateja wapya wa DStv wanaojiunga sasa na huduma hizo. 

Amesema mteja wa DStv anayelipia kifurushi cha juu ya kile anachotumia au cha mwisho kutumia atapandishwa kifurushi kwa muda wa mwezi mmoja bila malipo ya ziada na pia mteja mpya wa DStv aliyejiunga siku ya, au baada ya tarehe 8 Januari 2021 ambaye atalipia kifurushi cha juu ya kile alichojiunga nacho naye pia atanufaika na ofa hii. 

Hata hivyo, wateja wa DStv ambao wamelipia kifurushi chao kwa mwaka mzima hawahusiki na promosheni hii kwani hawa tayari wana ofa yao ambapo hupata mwezi mmoja wa kifurushi chao bila malipo ya ziada.  

Amefafanua kwamba Mteja atakayetaka kulipia kifurushi cha juu yake kabla kifurushi alichonacho hakijaisha naye atanufaika na ofa hii na pia salio lake la kifurushi cha awali litaendelea kubaki kwenye akaunti yake na hivyo kuwaza kulitumia tena punde ofa aliyopata itakapokamilika kulingana na vigezo na masharti.

Soma na hizi

Tupia Comments