Watu wengi hufikiri kuwa uzee huja pale umri unapokuwa mkubwa sana ambapo hupelekea mabadiliko ya mwili kama vile rangi ya nywele kuwa nyeupe, ngozi kuanza kujikunja, kuishiwa nguvu za mwili na mabadiliko mengine.
Unaambiwa Wanasayansi kutoka England wameeleza kuwa moyo wa mtu huwa miaka kumi zaidi ya umri halisi wa mtu huyo na inachangiwa na kutokula mlo kamili ‘Balance Diet’, kutofanya mazoezi na kuishi maisha hatarishi kama unywaji pombe kupita kiasi, kuvuta sigara, na kula vyakula vya kusindikwa na vyenye mafuta mengi.
Katika utafiti uliofanywa na Afya ya Jamii England imegundulika kuwa hili ni tatizo linalokuwa kwa kasi ulimwenguni kote ambapo 18% ya wanaume na 14% ya wanawake wenye miaka zaidi ya 50 huwa na moyo ambao unalingana na moyo wa mtu aliyewazidi miaka 10 jambo ambalo huwaweka kwenye hatari ya kupata maradhi kama kiharusi, mshtuko wa moyo, magonjwa sugu ya ini na kisukari.
Ulipitwa? SHAMBULIZI LA CHUI: Majeruhi asimulia alivyonusurika kuuawa
Rais Magufuli alivyokata tiketi na kupanda Pantoni…tazama kwenye hii video hapa chini!!!