Michezo

Hasira za Mwadui, Simba wamaliza kwa Mbeya City

on

Wekundu wa Msimbazi  Simba SC warejea kwa kishindo baada ya kuchapwa 1-0 na Mwadui FC, mtihani na hasira za kupoteza dhidi ya Mwadui, amekutana nao Mbeya City November 3 2019 uwanja wa Uhuru.

Simba SC wameiadhibu Mbeya City kwa kuwafunga magoli 4-0, magoli ya Simba SC yakifungwa na Meddie Kagere dakika ya 8, Clotous Chama dakika ya 43, Shiraf Shiboub dakika ya 77 na Deo Kanda aliyetokea benchi dakika ya 86.
.
Ushindi unaifanya Simba SC kujizatiti kileleni ukizinatia inaiacha Kagera Sugar nafasi ya pili kwa tofauti ya point 6, Simba SC wakiongoza kwa kuwa na point 21 wakati Kagera wakiwa na point 15.
KAPOMBE KAANIKA SABABU ZA KUSTAAFU KUICHEZEA TAIFA STARS

Soma na hizi

Tupia Comments