Michezo

Dube hauzwi 2024 “Ogopa matapeli”

on

Club ya Azam FC imeamua kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili mshambuliaji wao raia wa Zimbabwe Prince Dube na sasa atakuwepo Chamazi hadi 2024.

Dube alikuwa na mkataba wa miaka miwili ambao ulikuwa unamalizika 2022, Dune ndio kinara wa magoli Ligi Kuu Tanzania bara akiwa kafunga 14 ila kwa ujumla msimu huu ana magoli 17, matatu kati ya hayo amefunga kwenye Kombe la ASFC.

Dube alihusishwa kutakiwa na Simba SC, hivyo Azam FC baada ya kumtangaza rasmi kuongeza mkataba wameanza na tambo kwa kuandika “Ogopa Matapeli Dube hauzwi”

Dube akiwa na CEO wa Azam FC Abdulkarim Amin “Popat”

Soma na hizi

Tupia Comments