Mkali na Mkongwe kwenye Game, Dully Sykes amefunguka na AyoTVENT kuhusu Kuchelewa kuingia kwenye ndoa mpaka leo hii akiwa na miaka zaidi ya 40 ikiwa bado anafanya vizuri kwenye Muziki lakini haamini kuingia kwenye ndoa kwa sasa
Dully amezungumza hayo wakati akihojiwa kuhusu wimbo wake wa ‘Zali’ aliomshirikisha Alikiba, kufanya vizuri na kumrudisha kwenye trending ya music huku akisema amekuwa na heshima na Muziki Ndiomana ameendelea kufanya vizuri bila kuchuja tofauti na wasanii wengine
Mengine aliyoyaongea Dully Sykes ni kuhusu kuwashika mkono wasanii kama Marioo na Nandy ambao wamekuwa wakifanya vizuri kwa sasa na akituibia siri jinsi Marioo alivyokuwa akitaka apelekwe na Dully kwa Pfunk ili amuone Paula toka zamani kabla hajaja kuwa naye kwa sasa…