Mix

Ninazo nchi zinazokadiriwa kuja kuwa na watu wengi kufikia mwaka 2050! (Pichaz)

on

Dunia inabadilika kila siku mtu wangu, Dar es salaam ya leo pengine sio Dar es salaam ya kesho na ukweli huu ni sawa kwa kwa wenzetu wa Kenya, Uganda Rwanda na Burundi pia.

Umeshawahi kuivutia picha dunia ya mwaka 2050 na itakavyokuwa? idadi ya watu na maendeleo? vyote hivi ni muhimu kujiuliza na wengi wetu tunaweza hata tusiwepo mwaka 2050 ndio maana ‘The Population Reference Bureau’ imetoa ripoti inayoonyesha makadirio ya idadi ya watu kwenye nchi na miji tofauti kufikia mwaka 2050.

Ninazo hapa kwenye picha nchi 10 zinazokadiriwa kuja kuwa na watu wengi zaidi kufikia mwaka 2050Africa zipo nchi 3 tu!

Dunia2050

Idadi ya watu nchini Ethiopia ni milion 98.1 na kwa mujibu wa ripoti ya The Population Reference Bureau imekadiriwa kuwa kufikia mwaka 2050 Ethiopia itakuwa na idadi ya watu wasiopungua milion 165.

Dunia2050B

DRC Congo ni miongoni mwa nchi za Africa zilizotajwa, wakiwa milion 194 kwa sasa idadi ya watu Congo inakadiriwa kuongezeka mara mbili zaidi kufikia mwaka 2050.

DUNIA2050C

Bangladesh ni nchi ya 8 duniani inayoongoza kwa watu wengi, kwa sasa idadi yao inafika watu milion 202 lakini kufikia mwaka 2050 idadi ya watu Bangladesh inakadiriwa kubaki palepale.

DUNIA2050D

Brazil kwa sasa ina idadi ya watu wasiopungua milion 226, idadi kubwa ya watu nchini humo wakiwa watoto na kufikia mwaka 2050 Brazil inakadiriwa kuwa na idadi kubwa ya wazee duniani.

DUNIA2050E

Pakistan nayo imetajwa kwenye hesabu mtu wangu, idadi ya watu nchini humo kwa sasa inafika milion 344 lakini kwa mujibu wa ripoti yaThe Population Reference Bureau kufikia mwaka 2050 idadi ya watu Pakistan itapungua kufikia milion 199.

DUNIA2050F

Idadi ya watu Indonesia inagusa milion 366 lakini imekadiriwa kuwa kufikia mwaka 2050 Indonesia itakuwa na ongezeko la watu milion 110.

DUNIA2050G

Nigeria ni nchi nyingine kutoka Africa iliyoingia kwenye hesabu hii mtu wangu, idadi ya watu ikiwa milion 397, Nigeria imekadiriwa kufikia mwaka 2050 itakuwa nchi pekee yenye watu wengi Africa ya Kati.

DUNIA2050H

Marekani haiko nyuma sana, makadirio yanasema Marekani itaendelea kubakia nchi ya 3 yenye watu wengi zaidi duniani na uwezekano wao kubakia na idadi ile ile ya watu milion 398 mwaka 2050 ni kubwa.

BEIJING, CHINA - DECEMBER 14: (CHINA OUT) Job seekers pack a job fair for postgraduate students on December 14, 2008 in Beijing, China. Nearly 40,000 applicants competed for approximately 14,228 job positions at the fair. Chinese students are facing grimmer employment situation. The number of college graduates will hit 5.59 million this year, an increase of approximately 640,000 from 2007. Chinese students struggle to find positions with job vacancies becoming increasingly scarce due to the global economic crisis. (Photo by China Photos/Getty Images)

Kwa sasa China ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi zaidi duniani wakiwa na idadi ya watu bilion 1.366 lakini kufikia mwaka 2050 China inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wasiopungua bilion 1.42.

DUNIA2050J

India nayo inategemea kupata mabadiliko kufikia mwaka 2050, kwa sasa watu bilion 1.66 wanaibeba India lakini kufikia mwaka 2050 India inakadiriwa kuja kuwa nchi itakayoongoza kwa kuwa na watu wengi zaidi duniani.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments