Premier Bet
TMDA Ad

Stori Kubwa

Mpango ulivyosukwa kumtorosha muuza unga wa Mexico “El Chapo” gerezani! (Video)

on

chapo2

Headlines kubwa sasa hivi duniani na kwenye vyombo vingi vya habari ni kuhusiana na muuzaji sugu wa unga Joaquin Guzman maarufu kama El Chapo aliyetoroka jela siku chache zilizopita.

Stori nyingi zinaendelea kuibuka kwa uvumi mkubwa, maswali mengi pia yanaulizwa kuhusu kutoroka kwake na sasa hivi mke wake yupo mikononi mwa polisi wanaoamini kuwa kumkamata na kumuweka chini ya ulinzi kutawasaidia kujua maficho ya El Chapo yalipo.

chapo4

Serikali ya Mexico haijakaa kimya, imesema El Chapo ni adui namba moja wa umma sasa hivi na imetangaza kutoa zawadi ya dola Mil.3.8 sawa na Bil.7.2 za Kitanzania kwa mtu yoyote atakaetoa taarifa sahihi zenye uhakika za mahali alipo.

Hapa chini nimekusogezea baadhi ya videos zinazo onyesha njia aliyoitumia El Chapo kutoroka gerezani, ni shimo lililochimbwa chini kwa chini, kuna generator, taa za umeme na ukubwa wake hata bodaboda inaweza kupita mtu wangu!

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments