Mix

Mapenzi yana mambo, wivu ulitawala na kusababisha haya kwa huyu dada!

on

christy

Christy Sims ni mwanadada ambaye maisha yake yalibadilika ghafla baada ya aliekuwa mpenzi wake wa muda mrefu kumuachia majeraha ambayo hatokuja kuyasahau maishani.

Akiwa na miaka 40 Christy amelazimika kuishi na makovu baada ya kumwagiwa tindikali  na ex-boyfriend wake kwa sababu tu ya wivu wa mapenzi, kumhisi kuwa anatembea na mtu mwengine.

christy2

Christy Sims kabla ya tukio la kumwagiwa tindikali.

Haya yote yalitokea weekend moja ya mwaka 2013 nyumbani kwa mpenzi wake ambaye aliamua kumwagia dada huyu tindikali usoni, kifuani na mikononi kitendo kilichosukumwa na hasira kali za wivu.

Christy alipiga kelele nyingi na kuomba msaada lakini boyfriend wake aliamua kumuacha aungue mpaka watu wa huduma ya kwanza walipofika na kushangazwa kwa nini boyfriend huyo hakuchukua hatua za  kumpatia girllfriend wake huduma ya kwanza.

christy4

Christy Sims sasa hivi analazimika kuvaa miwani ya jua kila muda kulinda macho yake yasipigwe na jua la kumuumiza.

Jamaa alijitetea na kusema ilikuwa ni bahati mbaya lakini Mahakama imeona kuwa mwanaume huyo ana makosa 3, shambulio la kudhuru mwili, na makosa mengine mawili ambayo kwa yote atatumikia kifungo  miaka 60, miaka 20 kwa kila kosa.

 Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments