Mix

Habari Tatu kubwa kwenye TV za Tanzania leo July 10, 2017

on

Habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu ambapo kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya July 10, 2017 usijali millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tatu kubwa kupitia TV za Tanzania.

Habari ya Channel 10 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amesema kuwa watumishi wote wa umma waliobainika kutumia vyeti feki watachukuliwa hatua za kinidhamu pamoja na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Waziri Kairuki amesema hayo wakati wa mkutano wa watumishi wa Manispaa ya Temeke akisema hawatapata mafao kwa kuwa wamekuwa wakiisababishia Serikali hasara ya mimilioni ya fedha kwa kuwa walikuwa wanaidanganya kinyume na sheria ya utumishi wa Umma.

>>>”Wapo walionifuta wenyewe na kukiri kosa, wapo waliowatuma ndugu na wazazi wao. Baadhi ya watu wamekuwa wakidai walipwe na wengine wakitoa maoni mbalimbali. Nipende kuchukua fursa kupitia mkutano huu kuwaarifu watu wote waliobainika kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo katika utumishi wa Umma.” Angela Kairuki.

Habari ya Clouds TV

Wanachama na wapenzi wa Chama cha Wananchi CUF wamebaki na sintofahamu baada ya kuweka kambi ya zaidi ya saa nne ya kesi yao kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya DSM na kuamuriwa waondoke bila kujua kilichojiri baada ya muda wa Mahakama kuisha.

Kwa mujibu wa Clouds TV hadi saa Kumi na Moja jioni bado wanasheria wa pande zote mbili walikuwa hawajatoka jambo lililokuwa linaashiria kusikilizwa kwa kesi hiyo huku ulinzi ukiimarishwa nje ya Mahakama.

Habari ya TBC1

Waziri wa Fedha na Mipando Philip Mpango ameamuru kufungwa kituo cha mafuta cha Mawenzi kilichopo Kigamboni mpaka pale mmiliki wake atakapofinyia marekebisho kwenye kasoro zilizopo katika mashine za kutolea risiti zilizofungwa kwenye pampu za mafuta.

>>>”Mwambie boss wako, mimi na kutuma, mwambie Waziri wa Fedha ameagiza Kituo kifungwe kwa sababu hutumii mashine stahiki za EFD. Wewe toa taarifa tu, namba yangu ya nini? Waziri wa Fedha nchi hii yupo mmoja tu.” – Waziri Mpango.

“Sasa hivi tumeweka sheria mpaka majipu yanajitumbua yenyewe” – JPM

Soma na hizi

Tupia Comments